•Ifradi :Kufanya ibada ya hijja tu.
•Tamattui: Kufanya ibada ya hijja na umra na kutahalali (kuvua ihramu) baina ya ibada hizo.
•Qirani: Kufanya ibada ya hijja na umra kwa kuchanganya (bila ya kuvua ihramu).
i.MWEZI NANE:
•Utahirmia (rejea wajibu, sunna, yanayokatazwa kwa kwenye ihram).
•Mahala pa kuhirimia ni katika mikaat kwa anayefanya ifradi au qirani na Makka kwa anayefanya tamtui.
•Utaelekea Mina.
ii.MWEZI TISA:
•Utaelekea Arafa ( na kushikamana na adabu za kisimamo, sunna na wajibu wa kisimamo. Yanayofanywa Arafa.
•Utasali sala adhuhuri na laasiri kwa kuchanganya.
•Utaondoka Arafa baada ya jua kuchwa na kuelekea Muzdalifa.
•Utapitisha Muzdalifa (mabiitu) na kusali sala ya magharib na isha kwa pamoja.
•Utasali sala ya alfajiri na kuokota mawe.
iii.MWEZI KUMI:
•Utaondoka Muzdalifa na kuelekea Mina.
•Utapiga Jamaratul-Aqaba baada ya kuchomoza jua.
•Utanyoa au kupunguza nywele.
•Utachinja kwa uliyefanya tamatui au qirani.
NB. Ukimaliza utatahalali tahaluli ndogo.
•Utaelekea Makka na kufanya Tawaful-ifadha (tawafu ya nguzo).
•Utafanya saii (baina ya Safa na Marwa) iwapo unafanya tamattui na kwa anefanya Qirani au Ifradi atasai iwapo hakusai kwenye tawaful qudum.
N.B –Baada ya haya utakuwa umetahalul tahaluli ya pili na yote yaliyokuwa haramu kwa mwenye kuhirimia yatakuwa halali. Inajuzu kuahirisha tawafu hii hadi baada ya siku za kukaa mina kumalizika
•Utarejea Mina na kulala usiku wa mwezi kumi na moja.
MWEZI KUMI NA MOJA:
•Utarembea vijiwe Jamarati zote baada ya kuingia adhuhuri.
•Utalala Mina.
MWEZI KUMI NA MBILI:
•Utarembea vijiwe Jamarati zote tatu kama ulivyofanya mwezi (11).
•Hapo itajuzu kuondoka Mina kabla ya kuzama Jua. Likizama utawajibika kulala.
MWEZI KUMI NA TATU:
•Utapiga Jamarati tatu na kuondoka Mina.
TAWAFU YA KUAGA:
•Wakati wake ni mtu anapotaka kusafiri kurudi kwao.
•Hukumu yake ni wajibu na haitosamehewa ila kwa mwenye hedhi na nifasi iwapo watu waliofatana nao watataka kuondoka.
TANBIHI:
1.Anaekosa kukaa Arafat itamlazimu afanye Umra halafu achije na aje ailipe Hijja hiyo.
2.Asiewahi kufanya nguzo, hijja yake haitokubaliwa wala hatotahalali mpaka ailete nguzo hiyo.
3.Unapowacha wjiIbu itakubidi uchinje mbuzi usipopata utafunga siku 10, tatu ukiwa Makka na saba unaporudi nyumbani.
4.Unaponyoa au kukata kiasi cha nywele tatu kuendelea itakubidi utoe fidia ya mbuzi au utoe sadaka pishi sita kwa kila masikini pishi moja au ufunge siku tatu.
5.Unapozuiliwa kutimiza hijja au umra itakubidi uchinje mbuzi
6.Unapowinda itakubidi uchinje mfano wa mnyama uliyemuwinda au kulipa fidia kwa thamani yake na kununulia chakula ukitoe sadaka au kufunga kwa kila kibaba siku moja.